KLABU ya Barcelona na nyota wa Lionel Messi wameibuka washindi tena katika tuzo za Globe Soccer zilizofanyika huko Dubai jana, kwa kuondoka na zawadi ya timu na mchezaji bora. Messi alisafiri kutoka Argentina kwenda kuhudhuria sherehe hizo. Akihojiwa Messi amesema ni jambo zuri kupokea tuzo hiyo lakini kama asemavyo siku zote timu nzima ndio inafanya hilo kuwezekana.
Barcelona imefanikiwa kushinda mataji matano mwaka 2015 ambayo ni La Liga, Kombe la Mfalme, Ligi ya Mabingwa Ulaya, Super Cup ya Ulaya na Klabu Bingwa ya Dunia. Taji pekee ambalo wamelikosa kwa mwaka huu ni Super Cup ya Hispania ambalo lilikwenda kwa Athletic Bilbao.
Kocha wa timu ya taifa ya Ubelgiji Marc Wilmots ametajwa kama kocha bora wa mwaka huku Benfica ya Ureno wao wakichukua tuzo ya kuwa na shule bora ya soka. Viungo Andres Pirlo wa Italia na Frank Lampard wa Uingereza wao wamepewa tuzo kutokana na kucheza soka kwa kipindi kirefu zaidi.
No comments:
Post a Comment