Monday, December 28, 2015

MAN CITY YATAKA KUFANYA KUFURU KWA MESSI.

KLABU ya Manchester City inadaiwa kutenga kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili ya kumng’oa Lionel Messi kutoka Barcelona. Taarifa za gazeti la Sport zimedai wawakilishi wa Messi wamemuahidi kuwa atavuna kiasi cha paundi milioni 20 kwa msimu kama akitua City kiasi ambacho kinazidi kile anachopewa na mabingwa hao wa Hispania. Wakati Barcelona wakiwa hawana mpango wa kufanya mazungumzo ya mkataba mpya mpaka msimu ujao, klabu hiyo ina uhakika Messi ataikacha ofa hiyo kama alivyofanya wakati alipofuatwa na Paris Saint-Germain na Chelsea huko nyuma. Kwasasa City hawataweza rasmi ofa yao kwa Barcelona mpaka watakapoona dalili kwa Messi kuwa yuko tayari kukubali ofa yao.

No comments:

Post a Comment