Tuesday, December 29, 2015

VAN GAAL ADAI HANA SABABU YA KUJIUZULU.

MENEJA wa Manchester United, Louis van Gaal amesema haoni sababu ya kujiuzulu baada ya kikosi chake kutoka sare ya bila kufungana na Chelsea jana. United sasa wameshindwa kupata ushindi katika mechi nane za mashindano yote walizocheza ikiwa ni mara ya kwanza kutokea hivyo toka mwaka 1990 na wako nyuma kwa alama tano kufikia nafasi ya nne. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo Van Gaal amesema kama wachezaji wanaweza kucheza kwa kiwango kile wakiwa katika shinikizo hakuna sababu ya yeye kujiuzulu. Sare hiyo imeifanya United kuendelea kubaki katika nafasi ya sita katika msimamo wa Ligi Kuu ambayo inaendelea baadae leo kwa kuzikutanisha timu za Leicester City na Manchester City.

No comments:

Post a Comment