Tuesday, December 29, 2015

GUARDIOLA AKANUSHA KUTUMA UJUMBE WA CHUKI.

MSHAMBULIAJI aliyetimuliwa mara baada ya kusajiliwa na Barcelona, Sergi Guardiola amekanusha kutuma ujumbe katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter uliopelekea mkataba wake kusitishwa. Guardiola mwenye umri wa miaka 24 ni mmoja kati ya wachezaji watatu waliosajiliwa katika kikosi B cha Barcelona lakini ndoto zake za kuwachezea mabingwa hao wa Ulaya haraka zilizimika wakati ujumbe wa kuiponda klabu na kuhusu Catalonia ulipoonekana katika twitter yake. Katika taarifa rasmi, masaa machache baada ya kutangaza ujio wake, Barcelona walithibitisha kuwa wamebadili mawazo na kusitisha mkataba wake. Akihojiwa Guardiola amesema ameuelewa uamuzi wa klabu hiyo lakini amedai kuwa sio yeye aliyetuma ujumbe huo. Guardiola alianza kwa kuwaomba radhi Barcelona na Catalonia na kuendelea kudai kuwa ujumbe huo hakutumwa naye kwani kipindi cha mwaka 2013 ambacho ndio ujumbe unadaiwa kutumwa alikuwa hajui hata masuala hayo ya mitandao.

No comments:

Post a Comment