Tuesday, December 29, 2015

RONALDO AMPIGIA CHAPUO MESSI KUTWAA BALLON D'OR.

NGULI wa soka wa Brazil, Ronaldo amesema nyota wa Barcelona, Lionel Messi ni mchezaji aliyekamilika zaidi ya mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo. Wawili wapo katika orodha ya mwisho ya tuzo za Ballon d’Or sambamba na Neymar zawadi ambayo wamekuwa wakipokezana kwa miaka saba iliyopita huku Messi akishinda mara nne na Ronaldo mara tatu. Mjadala wa mchezaji gani ana kipaji zaidi ya mwenzake umekuwa ukitawala kwa kipindi kirefu, lakini Ronaldo ambaye naye ameshawahi kunyakuwa tuzo hiyo mara tatu amesema Messi ndio chaguo lake kati ya wawili hao. Ronaldo amesema amemchagua Messi kwasababu anamuona ni mchezaji aliyekamilika zaidi kuliko Ronaldo kwani anafanya vitu vyake kwa upekee.

No comments:

Post a Comment