MENEJA wa Arsenal, Arsene Wenger amemsifia Mesut Ozil kama mchezaji bora wa Ligi Kuu na kumfananisha na nguli wa klabu hiyo Dennis Bergkamp kufuatia kiwango kikubwa alichoonyesha katika ushindi wa mabao 2-0 waliopata dhidi ya Bournemouth jana. Kiungo huyo wa kimataifa wa Ujerumani, alitengeza bao moja na kufunga lingine katika mchezo huo uliofanyika katika Uwanja wa Emirates na kufanya timu hiyo kukwea kileleni mwa msimamo wa ligi. Mpaka sasa Ozil ameshatoa pasi za mwisho 16 na kufunga mabao matano katika ligi na kumfanya kukaribia rekodi ya pasi za mwisho 20 ambayo iliwekwa na nguli mwingine wa Arsenal Thierry Henry. Akihojiwa Wenger amesema ukitizama kiwango na idadi ya pasi za mwisho alizotoa msimu huu hakuna shaka kuwa ndio mchezaji bora kwasasa nchini Uingereza. Meneja huyo aliendelea kudai kuwa kiungo huyo kwasasa anakaribia kufanana na Bergkamp kwani pamoja na kutoa pasi lakini pia amekuwa akifunga mabao muhimu.
No comments:
Post a Comment