Tuesday, December 29, 2015

RUFANI YA MADRID YATUPILIWA MBALI.

KLABU ya Real Madrid, imeshindwa rufani yake ya kupinga kuenguliwa katika michuano ya Kombe la Mfalme kwa kuchezesha mchezaji asiyeruhusiwa. Mabingwa hao mara 19 wa michuano hiyo walienguliwa kwa kumchezesha winga Denis Cheryshev katika mchezo dhidi ya Cadiz uliochezwa Desemba 2 mwaka huu. Cheryshev alipaswa kutumikia adhabu yake kutocheza mechi moja ambayo aliipata wakati akicheza kwa mkopo Villarreal msimu uliopita. Mahakama ya Michezo ya Hispania ilitupilia rufani ya Madrid baada ya kusikiliza maelezo ya pande zote kuhusiana na sakata hilo. Madrid kwasasa wanashikilia nafasi ya tatu katika msimamo wa La Liga nyuma ya mahasimu wao Barcelona na Atletico Madrid.

No comments:

Post a Comment