Tuesday, December 29, 2015

SARE YAMRIDHISHA HIDDINK.

MENEJA wa muda wa Chelsea, Guus Hiddink ameridhishwa na sare ya bila kufungana waliyopata dhidi ya Manchester United jana, haswa kutokana na mabingwa hao wa Ligi Kuu kucheza bila mshambuliaji wa kueleweka. Diego Costa anatumikia adhabu baada ya kulimwa kadi Jumamosi iliyopita wakati walipotoa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Watford wakati Loic Remy na Radamel falcao wakiwa nje kutokana na majeruhi na kumlazimisha winga Eden Hazard kucheza katika nafasi asiyoizoea. Akihojiwa Hiddink amesema kiufundi walikuwa sawa na hata safu yao ya ulinzi ilikuwa imejipanga vyema. Hiddink aliendelea kudai kuwa hawakuwa na nguvu za kutosha kuiumiza United kwakuwa walikuwa na matatiz kidogo katika safu ya ushambuliaji kutokana na adhabu na majeruhi ya nyota wao.

No comments:

Post a Comment