Tuesday, December 29, 2015

IBE AIPA LIVERPOOL AHUENI.

MENEJA wa Liverpool, Jurgen Klopp amesema kiungo Jordon Ibe anaweza kurejea tena baada ya kupona katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Sunderland kesho. Hata hivyo, Klopp aliendelea kudai kudai kuwa pamoja na ahueni hiyo ya kurejea kwa Ibe lakini itabidi wasubiri wiki moja zaidi ili James Milner naye aweze kupona tayari kwa kurejea uwanjani. Ibe amekuwa benchi katika mechi mbili za ligi zilizopita za Liverpool akiokosa pia mchezo dhidi ya vinara Leicester City ambao walishinda kwa bao 1-0 Jumamosi iliyopita. Milner naye ameendelea kukaa nje kufuatia kupata majeruhi ya nyonga mapema mwezi huu. Akihojiwa Klopp amesema Ibe tayari ameshaanza mazoezi toka jana baada ya kuumwa kwa karibu wiki nzima, hivyo kuna uwezekano akawepo katika mchezo wa kesho.

No comments:

Post a Comment