Tuesday, December 29, 2015

UNITED YATENGA PAUNDI MILIONI 33 KWA KIUNGO WA LAZIO.

KLABU ya Manchester United imedaiwa kujipanga kutoa ofa ya paundi milioni 33 kwa ajili ya kiungo wa kushambulia wa Lazio, Felipe Anderson. Kwa mujibu wa taarifa zilizozagaa United walikuwa wamemuweka kiungo wa Real Madrid James Rodriguez katika rada zao lakini baada ya kuona uwezekano huo utakuwa mgumu kumsajili katikati ya msimu wameamua kugeuzia nguvu zao kwa Anderson. United wamejipanga kuongeza nguvu katika kikosi chao pindi dirisha dogo la usajili litakapofunguliwa mwishoni mwa wiki hii. Meneja wa United Louis van Gaal ambaye yuko katika shinikizo anataka kufanya mabadiliko ya haraka ili kikosi hicho kirejee katika hali ya ushindani kama walivyoanza msimu.

No comments:

Post a Comment