Sunday, December 27, 2015

WENGER AAPA KULIPA KISASI.

MENEJA wa Arsenal, Arsene Wenger amesema anaamini kikosi chake kitarudi vyema pamoja na kipigo kizito walichopata kutoka kwa Southampton jana wakati watakapoivaa Bournemouth kesho. Arsenal walibugizwa mabao 4-0 na Southampton katika Uwanja wa St Mary, na kushindwa kukaa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu. Pamoja na kipigo hicho Wenger anawaunga mkono wa wachezaji wake kuonyesha ukomavu katika mchezo wao unaofuata ili waweze kupata matokeo mazuri. Akihojiwa Wenger amesema wachezaji wake wana ari ya kipekee na watalionyesha katika mchezo wao ujao. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa wanataka kuondoka katika hali ya huzuni na anawaamini wachezaji wake wanaweza kufanya vyema kesho.

No comments:

Post a Comment