Sunday, December 27, 2015

MAJERUHI YAMNYIMA RAHA KOMPANY.

NAHODHA wa Manchester City, Vincent Kompany amejipambanua kama mtu asiyeonekana katika mchezo wa jana pamoja na kupata majeruhi dakika nane toka aingie. Beki huyo wa kimataifa wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 29 aliingia katika kipindi cha pili akitokea benchi katika ushindi wa mabao 4-1 waliopata City lakini alisalia uwanjani kwa dakika nane kabla ya kutolewa tena kutokana na majeruhi. Akihojiwa Kompany amesema jana ilikuwa siku mbaya kwake kwani alikuwa akijisikia fiti lakini anapata changamoto ya majeruhi madogo madogo. Beki huyo aliendelea kudai kuwa jambo hilo linamkera sana lakini atajitahidi kupambana ili aweze kurejea akiwa fiti zaidi.

No comments:

Post a Comment