Sunday, December 27, 2015

RAIS WA ATLETICO AMFUNGULIA COSTA MILANGO YA KURUDI.

RAIS wa Atletico Madrid, Enrique Cerezo amedai mshambuliaji wa Chelsea anaweza kurejea katika klabu hiyo siku zijazo. Nyota huyo wa kimataifa wa Hispania ameanza kurejea katika makali yake kufuatia kufunga mabao mawili katika sare ya mabao 2-2 waliyopata dhidi ya Watford katika mchezo wa Ligi Kuu. Costa mwenye umri wa miaka 27 amekuwa akihusishwa na tetesi za kurejea Atletico ambako ndio alikoanzia kabla ya kuhamia Uingereza Julai mwaka jana. Akiulizwa kuhusiana na suala hilo Cerezo hakuonyesha kukubali wa kukanusha kuwa nyota huyo anaweza kurejea Hispania. Cerezo amesema kwasasa Costa ni mchezaji wa Chelsea lakini huwezi kujua kinachoweza kutokea mbele katika soka.

No comments:

Post a Comment