KIUNGO wa kimataifa wa Ghana, Kevin-Prince Boateng amesajiliwa tena na klabu ya AC Milan kama mchezaji huru. Boateng amerejea San Siro kwa mkataba wa miezi sita mpaka mwishoni mwa msimu huu lakini ana nafasi ya kuongezewa mwingine. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 28 mzaliwa wa Ujerumani, ambaye mara ya kwanza aliiwakilisha Milan kati ya mwaka 2010 hadi 2013 amekuwa akifanya mazoezi na Milan toka Septemba mwaka jana. Boateng alisimamishwa katika klabu yake ya Schalke ya Ujerumani kutokana na makosa ya utovu wa nidhamu hivyo kumfanya kutocheza mechi yeyote toka kuanza kwa msimu huu.
No comments:
Post a Comment