MSHAMBULIAJI wa Liverpool, Daniel Sturridge anatarajiwa kuukosa mchezo wa mkondo wa kwanza wa Kombe la Ligi dhidi ya Stoke City baadae leo kufuatia kupata majeraha madogo akiwa mazoezini. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 26, amekuwa akisumbuliwa na majeruhi ya mara ya mara ambayo yamemfanya msimu uliopita kucheza mechi 19 na msimu huu mechi sita pekee. Meneja wa Liverpool, Jurgen Klopp ana mshambuliaji mmoja pekee Christian Benteke ambaye yuko fiti huku Divock Origi na Danny Ings nao pia wakiwa majeruhi. Kwa upande wa Stoke, Geoff Cameron atakuwepo katika mchezo wa kesho pamoja na kutolewa nje Jumamosi iliyopita. Beki huyo wa kimataifa wa Marekani alionyeshwa kadi nyekundu katika mchezo Ligi Kuu ambao Stoke walifungwa mabao 2-1 na West Bromwich Albion.
No comments:
Post a Comment