MSHAMBULIAJI nyota wa Gabon, Pierre-Emerick Aubameyang amesema amepata furaha isiyo na kifani kwa kufanikiwa kunyakuwa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa Afrika akiwashinda Yaya Toure wa Ivory Coast na Andre Ayew wa Ghana. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 26 anayekipiga katika klabu ya Borussia Dortmund anajivunia kuwa mchezaji wa kwanza kutoka Gabon kunyakuwa tuzo hiyo kubwa kabisa kwa Afrika baada ya kuonyesha kiwango kikubwa akiwa na klabu na timu yake ya taifa. Aubameyang amefafanua kuwa ushindi huo unamaanisha kuwa ukifanya kazi kwa bidii lazima utapata mafanikio unayotarajia na anaamini anaweza kutetea tena tuzo yake hiyo kwa mwaka huu. Pamoja na Aubameyang kumaliza mwaka uliopita bila taji lakini nahodha huyo wa Gabon alifunga mabao 29 huku akiwa tayari amefunga mabao 18 msimu huu. Wakati huohuo, Aubameyang amekanusha tetesi za kwenda Arsenal na kueleza hana mpango wowote wa kuondoka Dortmund kwasasa.
No comments:
Post a Comment