RAIS wa Shirikisho la Soka la Ulaya-UEFA aliyesimamishwa Michel Platini amesema hatasimama kugombea tena nafasi ya urais wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA mwezi ujao. Platini smbamba na rais wa FIFA Sepp Blatter wamefungiwa kujishughulisha na masuala yeyote ya soka kwa miaka nane. Wote wawili walikutwa na hatia kufuatia Blatter kufanya malipo yasiyoeleweka ya paundi milioni 1.3 kwenda kwa Platini mwaka 2011. Pamoja na wote kukata rufani kupinga kufungiwa kwao lakini Platini amesema hadhani kama muda utamtosha wa kuwahi uchaguzi huo utakaofanyika Februari 26. Platini aliendelea kudai kuwa ameamua kujitoa kwasababu kama ataweza kupambana kwa usawa kama ilivyo kwa wagombea wengine.
No comments:
Post a Comment