MAKELELE APEWA CHAVU MONACO.
KLABU ya Monaco ya Ufaransa, imemteua kiungo wa zamani wa Chelsea na Real Madrid, Claudio Makelele kuwa mkurugenzi mpya wa ufundi. Klabu hiyo ilitangaza jana uteuzi wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa, wakielezea kibarua chake kikubwa kitakuwa ni kumsaidia makamu wa rais Vadim Vasilyev kuongoza upande wa michezo wa timu hiyo. Makelele alitimuliwa kibarua cha kuinoa klabu ya Bastia Novemba 24 mwaka 2014 baada ya kufanya kazi kama kocha msaidizi katika klabu ya Paris Saint-Germain. Akihojiwa na mtandao wa klabu hiyo, Makelele amesema amefurahi kujiunga na klabu hiyo muhimu katika soka la Ufaransa na kuahidi kufanya bidii na kuisaidia timu hiyo.
No comments:
Post a Comment