Friday, January 15, 2016

FALCAO HUENDA AKAREJEA MONACO.

MAKAMU wa rais wa Monaco, Vadim Vasilyev amebainisha kuw aklabu hiyo inataka kumrejesha Radamel Falcao kutoka Chelsea alipo kwa mkopo lakini uhamisho huo unaweza kukwama kutokana na majeruhi yanayomsumbua. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 19 amefanikiwa kucheza katika mechi 10 toka ajiunge na mabingwa hao wa Ligi Kuu kiangazi mwaka jana na ameshindwa kufanya mazoezi huku Jose Mourinho akibainisha Novemba mwaka jana kuwa mshambuliaji huyo anasumbuliwa na matatizo ya misuli. Vasilyev sasa amebainisha kuwa wanamfuatilia Falcao ili kuwangalia uwezekano wa kumrejesha mwishoni mwa msimu. Makamu huyo wa rais amesema wamekuwa wakizungumza mara kadhaa na Falcao na kama sio majeruhi wangeweza kumchukua ili amalizie nusu ya pili ya msimu kipindi hiki cha Januari.

No comments:

Post a Comment