KLABU ya Central Coast Mariners imethibitisha kuwa Anthony Caceres amejiunga na Manchester City. Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 23 aliibuka katika kikosi cha kwanza cha klabu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu ya Australia mwaka 2013 na mpaka sasa amefunga mabao matau katika mechi 73 alizoichezea Mariners. Inaripotiwa kuwa mchezji huyo wa kimataifa wa Australia ambaye hajawahi kuitwa katika kikosi cha timu ya taifa, atapelekwa kwa mkopo katika klabu ya Melbourne City ambayo inamilikiwa na Manchester City. Kocha mkuu wa Mariners, Tony Walmsley amesema wanahitaji kusheherekea wakati wachezaji wa klabu hiyo wanaponunuliwa na klabu kubwa kwa ndio lengo lao kubwa.

No comments:
Post a Comment