TIMU ya mpira wa kikapu ya Toronto Raptors imefanikiwa kuichapa Orlando Magic kwa vikapu 106-103 katika mchezo wa Ligi ya Mpira wa Kikapu ya Marekani-NBA iliyofanyika katika Uwanja wa O2 Arena jijini London. Katika mchezo huo Kyle Lowry alifanikiwa kufunga alama 24 wakati DeMar DeRozan aliongeza zingine 13 na kudaka rebaundi 11 ambazo ziliiwezesha Raptors kupata ushindi wake wan ne mfululizo katika NBA.
Mchezo huo ni mmoja kati ya michezo sita ya NBA ambayo imekuwa ikichezwa jijini London kwa kadhaa iliyopita. Nyota wa Arsenal Alex Oxlade-Chamberlain na Olivier Giroud na nyota wa zamani wa Chelsea Didier Drogba ni miongoni mwa nyota waliohudhuria mchezo huo.


No comments:
Post a Comment