RAIS wa muda wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA, Issa Hayatou ameachia baadhi ya madaraka yake kama kiongozi wa Shirikisho la Soka la Afrika-CAF kufuatia kuongezeka kwa utata katika kampeni za uchaguzi wa shirikikisho hilo. Hayatou ataachia baadhi madaraka yake hayo kwa makamu wake wawili waliopo ili waweze kusimamia shughuli za CAF katika kipindi hiki ambacho yeye atakuwa zaidi akisimamia uchaguzi wa FIFA. Hatua hiyo imekuja ikiwa ni siku chache zimepita baada ya mgombea urais wa FIFA Prince Ali bin al Hussein wa Jordan kulalamikia hatua ya mashirikiano iliyowekwa na CAF pamoja na Shirikisho la Soka la Asia-AFC. Hata hivyo, maofisa wa CAF walikanusha kuwa hatua hiyo ya mashirikiano haina uhusiano wowote na suala uchaguzi wa FIFA ambao unatarajiwa kufanyika Februari 26 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment