Monday, January 18, 2016

SIONDOKI CITY - ZABALETA.

BEKI wa kulia wa Manchester City, Pablo Zabaleta ameondoa uwezekano wa kuondoka katika klabu hiyo katika kipindi hiki cha Januari baada ya vyobo vya habari vya Uingereza kumuhisisha na tetesi za kuhamia Inter Milan. Majeruhi mara mbili ya mguu aliyopata yamekuwa yakimkwamisha beki huyo mwenye umri wa miaka 31 msimu huu na kumfanya kucheza mechi yake ya tatu wakati ushindi wa mabao 4-0 waliopata dhidi ya Crystal Palace. Akihojiwa Zabaleta amesema anataka kumaliza msimu akiwa Etihad na hajafikiria lolote kuhusu kuondoka kipindi hiki. Zabaleta aliendelea kudai kuwa kwasasa anafanya bidii ili aweze kurejea katika nafasi yake na kuisaidia klabu katika malengo waliyojiwekea.

No comments:

Post a Comment