MENEJA wa muda wa Chelsea, Guus Hiddink anaamini klabu hiyo inastahili kumpa ofa ya mkataba mpya John Terry kwani anadhani beki huyo hajachuja toka alipowahi kumfundisha miaka saba iliyopita. Terry aliibuka shujaa katika mchezo wa Jumamosi iliyopita kufuatia kuifungia Chelsea bao la kusawazisha dakika za majeruhi katika mchezo dhidi ya Everton ambao ulimalika kwa sare ya mabao 3-3. Akihojiwa Hiddink amesema Terry ameonyesha umuhimu wake katika kikosi hicho kwani amekuwa akijituma kwa bidii pindi wanaposhabuliwa lakini pia wanaposhambulia. Meneja huyo aliendelea kudai kuwa hakuna tofauti kubwa kati ya Terry aliyemfundisha mwaka 2009 na huyu wa hivi sasa kwani bado anaonyesha kuwa nguvu na kasi pamoja na umri mkuwa alionao.
No comments:
Post a Comment