KLABU ya Atletico Madrid inaripotiwa kujipanga kumrejesha tena mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa. Vinara hao wa La Liga wamelimwa adhabu ya kutosajili na Shirikisho la Soka Duniani-FIFA ambayo itaanza kufanya kazi baada ya kumalizika kwa usajili wa dirisha dogo mwishoni mwa mwezi huu. Ingawa klabu hiyo imepanga kukata rufani lakini wanafahamu wanaweza kushindwa hivyo inabidi wafanye itakayoweza kuwasaidia ikiwemo kumrejesha Costa. Nyota huyo wa kimataifa wa Hispania aliondoka Atletico kueleka Chelsea mwaka 2014 na kufunga mabao 20 katika msimu wake wa kwanza lakini msimu huu amekuwa akisuasua.
No comments:
Post a Comment