Monday, January 18, 2016

GUARDIOLA KUMNG'OA SANCHEZ ARSENAL.

WINGA wa Arsenal, Alexis Sanchez anaripotiwa kuwa anaweza kuwa tayari kwenda Manchester United au Manchester City. Nyota huyo wa kimataifa wa Chile amekuwa kihusishwa na tetesi za kwenda Chelsea na Real Madrid katika miezi ya karibuni lakini winga huyo wa zamani wa Barcelona anadaiwa kuwa hataweza kwenda Chelsea. Hata hivyo anaripotiwa kuwa anaweza kuwa tayari kwenda katika klabu hizo za Manchester kama wataonyesha nia ya kumtaka. Na hatua hiyo itategemea zaidi kama Pep Guardiola atakwenda Old Trafford au Etihad, kwani Sanchez anapenda kufanya kazi tena na meneja huyo wa Bayern Munich baada ya kukaa vizuri wakiwa camp Nou.

No comments:

Post a Comment