
Monday, January 18, 2016
USHINDI DHIDI YA LIVERPOOL WAMPA JEURI VAN GAAL.
MENEJA wa Manchester United, Louis van Gaal amesema klabu hiyo bado iko katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu. United ambao walipata ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Liverpool jana wamekwea mpaka nafasi ya tano, wakitofautiana alama saba na vinara Arsenal pamoja na Leicester City wanaoshika nafasi ya pili. Akihojiwa Van Gaal amesema bado wana mechi nyingi zilizobakia hivyo watajitahidi kadri ya uwezo kupata matokeo mazuri ingawa anafahamu ugumu uliopo. United imewasogelea Arsenal na Leicester baada ya timu hizo kutoa sare mechi zao za mwishoni mwa wiki, ingawa Manchester City wanaoshika nafasi ya tatu na Tottenham Hotspurs ya nne wao walipata alama zote tatu. Van Gaal mwenye umri wa miaka 64 aliendelea kudai kuwa siku ya jana ilikuwa muhimu kwasababu washindani wao walipoteza alama hivyo kuwapa mwanya wa kuwakaribia kileleni.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment