Sunday, January 17, 2016

TETESI ZA USAJILI ZILIZOJIRI HUKO MAJUU.

KLABU ya Barcelona inatarajia kumsajili kiungo wa Arsenal, Aaron Ramsey majira ya kiangazi.
Chanzo: Daily Express

MENEJA mkongwe Sir Alex Ferguson anatarajiwa kutengua uamuzi wake wa kustaafu na kuja kumsaidia Ryan Giggs kufuatia tetesi za kutaka kutimuliwa kwa Louis van Gaal.
Chanzo: The People

KLABU ya Chelsea inaripotiwa kumtaja beki wa kati wa Crystal Palace Dann kama mchezaji atakayechukua mikoba ya John Terry Stamford Bridge pindi nahodha huyo wa zamani wa Uingereza atakapoondoka.
Chanzo: The People

KLABU ya Manchester United imepanga kutumia kitita cha paundi milioni 120 kwa ajili ya usajili wa kiangazi kuliko kufanya usajili wa Januari.
Chanzo: The People

KLABU ya Jiangsu Suning ya China inajipanga kutoa ofa ya mshahara wa paundi 230,000 kwa wiki kwa Yaya Toure na paundi milioni 10 kwa Manchester City kwa ajili ya kumnunua kiungo huyo.
Chanzo: Daily Star

No comments:

Post a Comment