Sunday, January 17, 2016

NIYONZIMA AIANGUKIA YANGA.

KIUNGO mahiri wa Yanga, Haruna Niyonzima hatimaye ameibuka hadharani na kuomba kuiomba radhi klabu hiyo kutokana na matatizo ya hapa na pale yaliyojitokeza baina yao. Nyota huyo wa kimataifa wa Rwanda alikuwa katika mgogoro na klabu hiyo hatua ambayo imepelekea kuondolewa katika kikosi cha timu hiyo kwa madai ya utovu wa nidhamu. Akizungumza na wanahabari leo katika makao makuu ya klabu hiyo, Niyonzima aliomba radhi kwa yote yaliyotokea na kuwataka viongozi wake kufikiria upya suala lake. Niyonzima ambaye tayari alitangazwa kutimuliwa na kudaiwa vidia ya mamilioni ya fedha na klabu hiyo, aliendelea kudai kikubwa kilichomleta hapa Tanzania ni kucheza soka ndio maana anataka masuala hayo yaishe ili aendelee na kibarua chake kama zamani. Naye ofisa habari wa Yanga, Jerry Muro amesema wamesikia maombi hayo na uongozi wa klabu hiyo utakutana ili kuona jinsi ya kulitatua tatizo la kiungo huyo.

No comments:

Post a Comment