Sunday, January 17, 2016

DEBUCHY ATAKA KUONDOKA ARSENAL.

BEKI wa Arsenal, Mathieu Debuchy amesema anahitaji kuondoka klabuni hapo katika kipindi hiki cha usajili wa Januari na kuna tetesi za kuwaniwa na klabu za Aston Villa na Bayer Leverkusen. Nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa amenyang’anywa nafasi yake katika kikosi cha kwanza na Hector Bellerin kufuatia majeruhi ya bega ya muda mrefu yaliyokuwa yakimsumbua msimu uliopita. Beki huyo wa zamani wa Newcastle United amecheza mechi saba pekee katika mashindano yote akiwa na Arsenal msimu huu na amesema kuondoka kwa mkopo au mkataba wa kudumu ni jambo analohitaji kwasasa. Akihojiwa Debuchy amesema ni kweli anataka kuondoka na kuna timu kadhaa zinazomuwania ila bado kwasasa anaangalia mahali gani patakapomfaa. Nyota huyo aliendelea kudai kuwa chochote kitakachotokea ikiwa hata kama kurejea tena Arsenal wakati wa kiangazi lakini lazima aondoke kipindi hiki ili aweze kupigania nafasi yake katika kikosi cha Ufaransa kwa ajili ya michuano ya Euro 2016.


No comments:

Post a Comment