Sunday, January 17, 2016

MARTINEZ ACHUKIZWA NA MWAMUZI KUIBEBA CHELSEA.

MENEJA wa Everton, Roberto Martinez amesema amekasirishwa baada ya kikosi chake kunyimwa ushindi kwa bao la kusawazisha lenye utata la Chelsea katika dakika ya 98 ya mchezo. Beki wa Chelsea ambaye alionekana akiwa ameotea aliisawazishia timu yake bao na kufanya mchezo kumaliza kwa sare ya mabao 3-3 katika Uwanja wa Stamford Bridge. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo, Martinez amesema waamuzi walifanya makosa makubwa kwani tayari muda wa nyongeza ulikuwa umemalizika na Terry aliotea wakati akifunga bao hilo. Martinez aliendelea kudai kuwa pengine waamuzi wanapaswa kusaidiwa kwani makosa kama hayo huwa yanagharimu timu haswa kikosi chake ambacho kilijitahidi kupambana ili kupata alama.

No comments:

Post a Comment