Sunday, January 17, 2016

RANIERI ATAKA ALAMA 79 MSIMU HUU.

MENEJA wa Leicester City, Claudio Ranieri ameweka mipango kwa kikosi chake kifikisha alama 79 msimu huu. Vinara hao wa Ligi Kuu wamefikisha alama 44 kufuatia sare ya bao 1-1 waliyopata dhidi ya Aston Villa jana hivyo kumaanisha Arsenal wanaweza kuwapita kama wakifanikiwa kuibuka na ushindi katika mchezo wao dhidi ya Stoke City baadae leo. Akihojiwa Ranieri amesema walifanikiwa kukusanya alama 39 katika nusu ya kwanza ya msimu na wanataka kuendelea kuimarika zaidi mwaka huu ili kufikisha zaidi ya alama 40. Kocha huyo amesema anafahamu itakuwa kazi ngumu lakini anadhani wanaweza kama wakiendelea kujituma kwa bidii zaidi.

No comments:

Post a Comment