Sunday, January 17, 2016

DINAMO ZAGREB YAIVIMBIA CHELSEA.

MENEJA wa Dinamo Zagreb, Zoran Mamic amethibitisha Chelsea wameshindwa kutoa ofa iliyohitajika kwa ajili ya kumsajili gokipa chipukizi Adrian Semper. Mapema wiki hii iliripotiwa kuwa mkurugenzi wa ufundi wa Chelsea Michael Emenalo alikwenda nchini Croatia kujaribu kufanya mazungumzo ya kumsajili kipa huyo mwenye umri wa miaka 18. Hata hivyo, pamoja na kutoelezea kwa undani kilichoendelea katika mzungumzo hayo, Mamic amefafanua kuwa ofa ya Chelsea ilikataliwa. Mamic amesema pamoja na ofa nzuri iliyotolewa na Chelsea lakini waliikataa kwasababu haikufikia malengo waliyotaka.

No comments:

Post a Comment