MENEJA wa Chelsea Guus Hiddink amebainisha kuwa Diego Costa alikimbizwa hospitali baada ya kupata majeruhi katika ugoko kufuatia sare ya mabao 3-3 waliyopata dhidi ya Everton jana. Akihojiwa Hiddink amesema Costa alikimbizwa hospitali ili kufanyiwa vipimo na wana matumaini halitakuwa tatizo kubwa sana kwani aliondoka akiwa na maumivu makali katika mguu wake. Costa mwenye umri wa miaka 27 nafasi yake ilichukuliwa na Loic Remy katika dakika ya 80 ya mchezo baada ya kujiumiza mwenyewe wakati akichuana na Leighton Baines. Nyota huyo wa kimataifa wa Hispania mzaliwa wa Brazil alianza msimu huu kwa kusuasua lakini amefanikiwa kufunga mabao matano katika mechi tano zilizopita za Chelsea na kumfanya kufikisha mabao tisa katika mashindano yote msimu huu.

No comments:
Post a Comment