NAHODHA wa Manchester City, Vicente Kompany amenusurika wakati ndege ndogo aliyokuwa amepanda ilipotoka nje ya barabara wakati ikijaribu kuruka. Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa ndege hiyo ilikwenda kusimama katika majani katika Uwanja wa Ndege wa Norwich na hakuna yeyote aliyeumia katika tukio hilo. Beki huyo wa kimataifa wa Ubelgiji alikuwa amekwenda katika mji huo kushuhudia mchezo kati ya City na Norwich City ambao ulimalizika kwa timu yake kushinda mabao 3-0 na kusonga mbele katika mzunguko wa nne wa Kombe la FA. Kompany ambaye anadaiwa kuwa na watu wengine watano kwenye ndege hiyo, hakucheza katika mchezo huo kutokana na kuendelea kuuguza majeruhi ya nyonga.
No comments:
Post a Comment