Monday, January 11, 2016

BLATTER KUPINGA ADHABU YAKE RASMI.

WAKILI wa aliyekuwa rais wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA, Sepp Blatter amethibitisha jana kuwa atawasilisha rufani yao kupinga adhabu ya kufungiwa miaka nane aliyopewa mteja wake. Hatua hiyo imekuja kufuatia kamati ya nidhamu ya FIFA kubainisha juzi kuwa itawasilisha sababu zilizopelekea kufungiwa kwa Blatter na rais wa Shirikisho la Soka la Ulaya-UEFA, Michel Platini, hivyo kutoa mwanya kwa wawili hao kukata rufani. Wakili wa Platini ambaye pia amefungiwa miaka nane naye alithibitisha mapema kuwa watawasilisha rufani yao. Rufani za Blatter na Platini zilikuwa zikitegemewa kwani wawili hao mara kadhaa wameapa kusafisha majina yao kufuatia sakata hilo. Desemba mwaka jana FIFA iliwachukulia adhabu hiyo viongozi hao kwa kutumia nyadhifa zao vibaya kufuatia malipo ya paundi milioni 1.3 aliyopewa Platini mwaka 2011 kwa kazi zilizofanyika kti ya mwaka 1999 na 2002.

No comments:

Post a Comment