Wednesday, January 13, 2016

ORIGO KUFANYIWA UPASUAJI WA GOTI.

MENEJA wa Liverpool, Jurgen Klopp amethibitisha kuwa mshambuliaji Divock Origi anatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa goti. Nyota huyo wa kimataifa wa Ubelgiji, amefunga mabao manne katika mshindano yote akiwa na Liberpool msimu huu lakini hajacheza toka Desemba 26 wakati alipopata majeruhi ya msuli wa paja katika mchezo dhidi ya Leicester City. Klopp amebainisha kuwa klabu hiyo imeamua kutumia muda ambao atakuwa akijiuguza msuli kutibu tatizo lingine lililokuwa likimkabili nyota huyo mwenye umri wa miaka 20 na anatarajiwa kurejea uwanjani Februari. Akihojiwa meneja huyo amesema upasuaji huo hautakuwa mkubwa lakini utasaidia kurekebisha tatizo la goti lililokuwa likimsumbua.

No comments:

Post a Comment