Thursday, January 14, 2016

SHAQIR MGUU NJE MGUU NDANI MCHEZO WA ARSENAL.

MSHAMBULIAJI wa Stoke City, Xherdan Shaqir yuko katika hatihati ya kuukosa mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Arsenal Jumapili hii kutokana na majeruhi ya msuli wa paja. Nyota huyo wa kimataifa wa Uswisi alilazimika kutolewa nje katika mchezo dhidi ya Norwich City jana ambao walishinda kwa mabao 3-1 na meneja Mark Hughes ameweka wazi kuwa kuna hatihati kwa Shaqir kuukosa mchezo huo. Akihojiwa Hughes amesema kwa jinsi anavyohisi Shaqir anaweza kukaa nje ya uwanja kwa karibu siku 10 hivyo ni wazi hataweza kuwepo mchezo wa Jumapili. Pamoja na hilo Hughes ana uhakika kikosi chake kipo imara tayari kwa ajili ya mchezo huo muhimu.

No comments:

Post a Comment