Thursday, January 14, 2016

WENGER ATHIBITISHA KUMNASA KIUNGO WA FC BASEL.

MENEJA wa Arsenal, Arsene Wenger amethibitisha kumsajili kiungo wa Fc Basel Mohamed Elneny ambaye anaweza kumtumia katika mchezo dhidi ya Stoke City Jumapili hii. Elneny mwenye umri wa miaka 22, ameiripotiwa kuigharimu klabu hiyo kitita cha paundi milioni tano na anaruhusiwa kucheza katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Akihojiwa mara baada ya Arsenal kupata sare ya mabao 3-3 dhidi ya Liverpool jana, Wenger alithibitisha taarifa hizo na kuongeza kuwa anawez akumtumia kumtumia katika mchezo dhidi ya Stoke. Elneny alikuwa akiichezea Basel wakati walipoibuka na ushindi dhidi ya Chelsea msimu wa 2013-2014.

No comments:

Post a Comment