Monday, January 18, 2016

WATFORD YAMCHUKUA NYOTA WA MOROCCO.

KLABU ya Watford imemsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Morocco Nordin Amrabat kutoka klabu ya Malaga ya Hispania. Amrabat mwenye umri wa miaka 28 alikuwa kwa mkopo msimu uliopita katika klabu hiyo ya La Liga kabla ya kusaini mkataba wa moja kwa moja na kuitumikia mechi 15 msimu huu. Nyota huyo mzaliwa wa Uholanzi alianza kuichezea timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 21 ya nchi hiyo kabla ya kuamua kuichezea Morocco. Meneja wa Watford Quique Sanchez Flores amesema Amrabat ana ubora wa wachezaji ambao wanawahitaji hivyo anadhani atawasaidia katika malengo yao.

No comments:

Post a Comment