KLABU ya Barcelona jana ilifanikiwa kuweka rekodi mpya ya kutofungwa mechi 29 baada ya kupata sare ya bao 1-1 dhidi ya Valencia na kutinga fainali ya Kombe la Mfalme. Rekodi iliyokuwepo ya kutofungwa mechi 28 iliwekwa katika msimu wa 2010-2011 chini ya Pep Guardiola lakini kikosi cha sasa kilicho chini ya Luis Enrique kilifikia rekodi hiyo katika mchezo wa Jumapili iliyopita walioshinda mabao 2-0 dhidi ya Levante. Matokeo hayo ya jana yanaifanya Barcelona kupata ushindi katika mechi 23 na kutoa sare sita toka walipofungwa mara ya mwisho na Sevilla katika mchezo uliochezwa Octoba 3 mwaka jana. Katika kipindi chote hicho Barcelona imefanikiwa kufunga mabao 87 na kuruhusu kufungwa 15 pekee huku Luis Suarez akiongoza orodha ya wafungaji kwa kuwa na mabao 30 akifuatiwa na Lionel Messi mwenye mabao 18. Mchezo unaofuata wa Barcelona utakuwa dhidi ya Celta Vigo ambao wanapambana na Sevilla baadae usiku.
No comments:
Post a Comment