KLABU za Bayern Munich na Borussia Dortmund zinaweza kukutana katika hatua ya fainali ya michuano ya DFB-Pokal baada ya timu hizo kupangwa tofauti katika hatua ya nusu fainali. Baada ya kushinda mabao 3-0 dhidi ya Bochum katika hatua ya robo fainali, Bayern sasa wamepangiwa kucheza nyumbani dhidi ya Werder Bremen kwenye hatua ya nusu fainali. Bayern iliyo chini ya Pep Guardiola watakuwa wakifukuzia taji lao la 18 katika historia ya michuano hiyo. Dortmund wao watakwaana na Hertha Berlin ambao waliponea chupuchupu kutolewa na FC Heidenheim katika hatua ya robo fainali.
No comments:
Post a Comment