Thursday, February 11, 2016

BLANC AJITIA KITANZI PSG.

MENEJA wa Paris Saint-Germain Laurent Blanc amesaini mkataba mpya ambao utamuweka katika klabu hiyo mpaka mwaka 2018. Beki huyo wa zamani wa Ufaransa alichukua mikoba ya kuinoa PSG kutoka kwa Carlo Ancelotti June mwaka 2013 na kuingoza timu hiyo kushinda mataji mawili ya ligi, ikiwemo mataji matatu ya dani msimu uliopita. PSG kwasasa wanaongoza ligi kwa tofauti ya alama 24 wakiwa hawajafungwa mechi yeyote msimu huu na wanatarajiwa kuchuana na Chelsea katika hatua ya mtoano ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Akihojiwa mara baada ya kusaini mkataba huo, Blanc aliwashukuru viongozi kwa kuweka imani dhidi yake na kuahidi kuendeleza mazuri zaidi katika timu hiyo.

No comments:

Post a Comment