TAKWIMU mpya zilizotolewa zimebainisha kuwa klabu za Ligi Kuu zimetumia zaidi ya paundi bilioni moja katika usajili wa msimu mmoja kwa mara ya kwanza. Kiasi cha paundi milioni 965 kilivunja rekodi ya msimu wa 2014-2015, lakini tayari rekodi hiyo imeshapitwa huku klabu bado zikiwa na muda wa kusajili wachezaji zaidi mpaka ifikapo leo saa sita usiku dirisha litakapofungwa. Klabu 20 za Ligi Kuu tayari zimeshatumia paundi milioni 130 katika kipindi hiki cha usajili wa Januari pekee, huku Newcastle United ndio klabu iliyotumia fedha nyingi zaidi mpaka sasa wakitumia paundi milioni 29. Klabu hiyo imewasajili Jonjo Shelvey, Andros Townsend na Henri Saivet huku wakiwa tayari wametuma maombi ya paundi milioni 21 kwa ajili ya kuwania mshambuliaji wa West Bromwich Albion Saido Berahino.
No comments:
Post a Comment