Wednesday, February 17, 2016

LAVEZZI NAYE ATIMKIA CHINA.

KLABU ya Hebei China Fortune imetangaza kumsajili winga wa Paris Saint-Germain-PSG Ezequiel Lavezzi. Mkataba wa nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa ulikuwa unamalizika mwishoni mwa msimu huu ambapo badala ya kuangalia uwezekano wa kuongeza mwingine ameamua kwenda kucheza soka nchini China kwa kitita kinachokaridiwa kufikia euro milioni nne. Mbali na hilo pia Lavezzi anategemewa kupewa mshahara wa euro milioni 10 kwa msimu pamoja na malipo mengine ya bakshishi yanayofikia euro milioni sita. Klabu hiyo mpya ambayo imepanda daraja msimu uliopita ilitangaza dili hilo kupitia mtandao wake.

No comments:

Post a Comment