Wednesday, February 17, 2016

LEWANDOWSKI KUONGEZA MKATABA NA BAYERN.

MSHAMBULIAJI wa Bayern Munich, Robert Lewandowski anadaiwa kuwa tayari kuongeza mkataba na klabu hiyo na kukataa fedha nyingi kutoka klabu za Ligi Kuu. Nyota huyo kwasasa ana mkataba na mabingwa wa Bundesliga ambao unamalizika Juni mwaka 2019 lakini ameendelea kuhusishwa na tetesi za kuhamia mahali kwingine na wakala wake amethibitisha hivi karibuni kuwa mazungumzo ya mkataba mpya yanakaribia kuanza. Akihojiwa mashambuliaji huyo amesema anafahamu kuwa kuna klabu zinamuhitaji nje ya Ujerumani lakini ana uhakika kuwa ataongeza mkataba mwingine na Bayern kwasababu ya timu bora waliyonayo. Lewandowski amesema haoni sababu ya kuondoka kwasababu ameona jinsi gani klabu hiyo inavyojiandaa kwa siku zijazo.

No comments:

Post a Comment