BEKI wa kushoto wa Atletico Madrid Filipe Luis amepunguziwa adhabu ya kutocheza mechi tatu aliyopewa mpaka kubakiwa na mechi moja pekee. Filipe alilimwa adhabu hiyo kufuatia kuchezea hovyo mshambuliaji nyota wa Barcelona Lionel Messi katika mchezo baina ya timu hizo ambao ulimalizika kwa Atletico kupigwa mabao 2-1. Beki huyo alilimwa kadi nyekundu katika mchezo huo uliochezwa mwishoni mwa wiki iliyopita na kusababisha meneja wa Barcelona Luis Enrique kulalamika. Rufani ya Atletico ilifanikiwa baada ya jopo la Kamati ya Rufani ya Shirikisho la Soka la Hispania kukutana na kuamua kumpunguzia adhabu Filipe. Hata hivyo, Atletico bado wana matatizo katika safu yao ya ulinzi wakati wakielekea katika mchezo wao wa kesho dhidi ya Eibar kutokana na Diego Godin na Juanfran kutumikia adhabu huku Stefan Savic akiwa majeruhi.
No comments:
Post a Comment