BABA wa mshambuliaji nyota wa Barcelona, Neymar amedai Manchester United imetenga kitita cha paundi milioni 144 kwa ajili ya kumuwania nyota huyo majira ya kiangazi. United wako tayari kutoa ada hiyo itakayovunja rekodi ili waweze kuvunja mkataba wa nyota huyo wa kimataifa wa Brazil lakini klabu na mchezaji wamenyamaza kimya huku baba yake Neymar Senior akiamini mwanae ataendelea kubaki Camp Nou kwa kipindi kirefu kijacho. Akihojiwa mzee huyo amesema United wako tayari kutoa paundi milioni 144 kwa ajili ya kumsajili mwanae lakini hadhani kama hilo litawezekana kwakuwa mwanae bado ana mkataba wa miaka miwili na anafurahia maisha ya Barcelona. United walitumia zaidi ya paundi milioni 108 katika usajili wa majira ya kiangazi uliopita huku ikiuza wengine akiwemo Angel Di Maria aliyekwenda Paris Saint-Germain.
No comments:
Post a Comment