Wednesday, February 3, 2016

YAYA TOURE KUVUNA MAMILIONI AKIENDA CHINA.

GAZETI la Daily Telegraph limedai kuwa Yaya Toure anaweza kupata paundi milioni 30 kwa msimu kama akiamua kuondoka Manchester City na kwenda kucheza Ligi Kuu ya China. Kiungo huyo wa kimataifa wa Ivory Coast mustakabali wake uko mashakani kufuatia kuthibitishwa kwa ujio wa Pep Guardiola majira ya kiangazi, kwani ndio kocha aliyemuuza wakati akiwa Barcelona. Kwa mujibu wa watu wa karibu Toure wamedai nyota huyo anataka kuendelea kubakia City lakini anaweza kulazimishw akuondoka kama Guardiola akiamua kuwekeza kwa kufanya usajili mpya katika nafasi yake. Klabu tatu za China ikiwemo Jiangsun Suning zimeshaonyesha nia ya kutaka kumsajili kiungo huyo mwenye umri wa miaka 32 na wanaweza kumfanya kuwa mchezaji anayelipwa zaidi baada ya Lionel Messi na Cristiano Ronaldo.

No comments:

Post a Comment