MAHAKAMA nchini Brazil imezuia baadhi ya mali za mshambuliaji nyota wa nchi hiyo Neymar. Mahakama ya shirikisho iliyopo jijini Sao Paulo ilitangaza kutoa hati ya kuzuia mali zenye thamani ya karibu paundi milioni 34.5 ambazo zinamilikiwa na nyota huyo wa Barcelona. Baadhi yake ni boti ya kifahari, ndege binafsi na mali nyingine kadhaa ikiwemo kampuni tatu ambazo zinamilikiwa na familia yake. Neymar mwenye umri wa 23 anatuhumiwa kukwepa kodi kati ya mwaka 2011 na 2013 na anakabiliwa na mashitaka ya kisheria ingawa mwenye alikanusha kufanya jambo lolote baya.
No comments:
Post a Comment